The House of Favourite Newspapers

Rufaa ya Mbowe Ngoma Nzito, Wawekewa Pingamizi (Picha +Video)

Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa barabarani wakati basi la Magereza likiwarudisha rumande Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

RUFAA ya dhamana ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko imesikilizwa leo asubuhi Alhamisi Novemba 29, 2018, katika Mahakama Kuu  Dar es Salaam chini ya Jaji Sam Rumanyika, imeshindikana kutolewa uamuzi leo hadi kesho.

Akizungumza baada ya kusikiliza hoja za kisheria juu ya watuhumiwa hao kupatiwa rufaa Jaji Rumanyika amesema atazipitia hoja zote za pande mbili ili  kujiridhisha hivyo atatoa uamuzi wa rufaa hiyo kesho saa nne.

Rufaa ya kesi hiyo ilifunguliwa baada ya kesi  inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana kwenye kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Mtangazaji wa Global TV, Lucas Masungwa, akiwa eneo la mahakama.

 

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Vicent Mashinji akiongea na wanahabari, amesema kuwa mahakama imeamua kesho itatoa maamuzi baada ya  upande wa mashtaka kuwasilisha pingamizi la awali wakiomba rufaa hiyo itupiliwe mbali wakitoa hoja tatu za kisheria.

Kufuatia hilo mahakama imeamua kuanza kusikiliza pingamizi hilo kabla ya kuendelea na rufaa.

 

(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA | GPL)

 

Comments are closed.