The House of Favourite Newspapers

Rugemarila Azua Mapya Sakata la Escrow, Sasa Kumtaja Mwizi wa Fedha za Escrow

MFANTABIASHARA hara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwamba anataka aonane na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampatie ushahidi wa mtu anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.

 

Rugemarila alianza kuieleza mahakama December 8, 2017 unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh bilioni 309 za serikali anazoshtakiwa nazo ambapo leo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo akaomba kuahirishwa kwa kesi hiyo ili waendelee kukamilisha upelelezi jambo ambalo Rugemarila alinyoosha mkono na kusema anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano kisha kumrudisha salama gerezani.

“Leo nimekuja na ushahidi, naomba nionane na DPP ili nimsaidie kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent (hatuna hatia),” alieleza Rugemarila.

Baada ya maelezo hayo ya Rugemarila, Hakimu Shaidi kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua na kuwasilisha kwa DPP kuhusu jambo hilo huku akiihirisha kesi hiyo hadi January 5, mwakani.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Dola 22.

Comments are closed.