The House of Favourite Newspapers

Ruvuma: Polisi Wadaiwa Kumchoma Singe Mwenyekiti wa Kijiji

0

MWENYEKITI wa ulinzi wa Kijiji cha Peramiho A, mkoani Ruvuma ambaye pia ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtakuja, Pastorius Mbuya, amejeruhiwa kwa kipigo cha askari polisi waliochukizwa na mwenyekiti huyo kumpigia simu mkuu wao wa kazi na kuwagongea usiku wakati kituo cha polisi kimefungwa.

 

Mbuya alienda kituoni hapo saa sita usiku akiwa na kijana ambapo polisi walikataa kumshughulikia baada ya kukuta kituo cha polisi kimefungwa, hivyo kitendo cha kugonga kiliwachukiza askari hao ndipo wakampiga na kumchoma singe ya bunduki mguuni na mkononi.

 

Dereva wa bodaboda, Alifa Ausi, aliyempeleka ,Mbuya kituo cha polisi kushughulikia suala la mwanafunzi, anasema alishuhudia polisi wakimtukana matusi mwenyekiti wa kitongoji kabla ya kumpa kipigo kilichomjeruhi.

 

Mkuu wa wilaya ya Songea, Pololet Mgema, amesema atalifuatilia suala hilo na kuchukua hatua kwa kuwa linaondoa imani ya jeshi la polisi kwa wananchi.

 

Akizungumza kwa simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, ACP Simon Marwa,  amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa liko kwenye uchunguzi.

 

Leave A Reply