The House of Favourite Newspapers

Wachina Waliotaka Kumhonga Kamishna TRA Wahukumiwa

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47) kulipa faini ya Tsh. Milioni 1 kila mmoja.

Pamoja na hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi, baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa rushwa, pia Mahakama imetaifisha pesa zao kiasi cha Tsh. Milioni 11.5 ambazo walitaka kumhonga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Edwin Muhende kabla ya kuwashtukia na kuita maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Watu hao walilipa faini hiyo na kuachiliwa huru.

Leave A Reply