The House of Favourite Newspapers

Ruvuma: Viongozi wa Chadema Waliokamatwa, Waachiwa Huru

1
Viongozi wa Chadema (Picha na Maktaba).

 

NYASA, RUVUMA: Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wengine sita wa chama hicho waliokamatwa juzi kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali na Jeshi la Polisi wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma leo, saa tano asubuhi wameachiwa huru kwa dhamana.

 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu, Julai 17, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene, imeeleza kuwa viongozi hao waliachiwa baada ya chama hicho kuzitaka mamlaka zilizohusika kuwakamata kutoa amri ya kuwaachia huru.

 

“Jana tulizitaka mamlaka zilizohusika kutoa amri ya kuwakamata zitoe amri ya kuwaachia huru mara moja kabla chama hakijatoa kauli nyingine kuhusu hatua zingine ambazo kingechukua kulinda sheria, uhuru na haki katika nchi,” amesema Makene katika taarifa hiyo.

 

Juzi Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Kamishna Gemini Mushi alizungumza na Mwananchi na kueleza kuwa viongozi hao walikamatwa baada ya kufanya maandamano wakati waliomba kibali cha kufanya kikao cha ndani.

 

Viongozi waliokuwa wamekamatwa ni Katibu Mkuu Vincent Mashinji, Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo aliyopewa ODC wa Nyasa kuwakamata viongozi hao na kuwaweka selo kwa saa 48.

Wengine waliokuwa wamekamatwa ni;

1. Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda)
2. Ireneus Ngwatura (M/kiti Mkoa)
3. Delphin Gazia (Katibu Mkoa)
4.Asia Mohamed (Afisa Kanda)
5. Cuthbert Ngwata (M/kiti Wilaya)
6. Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya)

Kwa mujibu wa taarifa ya awali, polisi walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk. Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.

 

Lowassa Aliporipoti kwa DCI Kuhojiwa kwa Mara ya 3

1 Comment
  1. […] Ruvuma: Viongozi wa Chadema Waliokamatwa, Waachiwa Huru […]

Leave A Reply