The House of Favourite Newspapers

Rwanda kuruhusu wageni kutoka mataifa ya Afrika kuingia bila Visa

0

Rwanda Alhamisi wiki hii ya Novemba 2023 imetangaza kwamba itawaruhusu waafrika kuingia nchini humo bila ya visa, likiwa taifa la karibuni la katika bara hilo kuchukua hatua inayolenga kuimarisha usafiri wa watu na bidhaa, sawa na ilivyo barani Ulaya kwenye eneo la Schengen.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, rais wa taifa hilo Paul Kagame alitoa tangazo hilo katika mji mkuu wa Kigali, ambapo alihimiza uwezo wa Afrika kama kivutio cha utalii wa ndani, kinyume na kutegemea asilimia 60 ya watalii kutoka nje, kulingana na data kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Afrika.

Muafrika yeyote anaweza kuchukua ndege na kuingia Rwanda pale anapotaka, bila kulipia chochote, amesema Kagame wakati wa kongamano la 23 la Kimataifa la Baraza la Usafiri na Utalii. Iwapo hilo litatekelezwa, Rwanda itakuwa taifa la nne la kiafrika kutangaza hatua hiyo baada ya Gambia, Benin, na Ushelisheli.

Rais wa Kenya William Ruto mapema wiki hii alitangaza mpango wa kuruhusu waafrika kutembelea taifa hilo la Afrika Mashariki bila kulipia visa, ifikapo Decemba 31.

ESTER BULAYA AMVAA SIRRO AZITAPIKE BIL4 ZILIZOPOTEA-”ARUDISHWE ABEBE MZIGO WAKE, ALIWAPA WASHKAJI”

Leave A Reply