The House of Favourite Newspapers

Rwanda Yaanza Kutengeneza Magari ya Volkswagen – Pichaz

RAIS Paul Kagame amezindua kiwanda kipya cha kampuni maarufu ya magari ya Volkswagen nchini Rwanda, leo Juni 27, 2018 ambapo uzalishaji wa magari hayo umeanza rasmi nchini humo.

Kampuni hiyo maarufu ya kutengeneza magari yenye makao yake makuu nchini Ujerumani, imeamua kuwekeza nchini Rwanda ili kuwarahishia wateja wake upatikanaji wa bidhaa hiyo, kukuza soko lake Afrika Mashariki, Kati na Afrika nzima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulioendana na kuzindua gari la kwanza lililotengenezwa na kiwanda hicho cha Volkswagen nchini Rwanda, Kagame amesema fursa hiyo siyo tu ni ya kuongeza viwanda nchini humo bali itakuwa na manufaa ya kutengeneza ajira nyingi miongoni mwa Wanyarwanda.

 

Aidha, mbali na kuunganisha magari hayo (assembling) kiwanda hicho pia kitakuwa kikitengeneza spea za magari hayo na vifaa vingine vya Volkswagen.

Magari yatakayoanza kutengenezwa na Volkswagen kwa sasa ni aina ya Hatchback Polo, Passat na Teramont.

Comments are closed.