The House of Favourite Newspapers

Rwanda Yataka Rwigara, Mama’ke Wafungwe Miaka 22

Diane Shima Rwigara.

UPANDE wa mashitaka nchini Rwanda umeitaka Mahakama Kuu ya Kigali kutoa adhabu ya kifungo cha miaka 22 jela kwa Diane Shima Rwigara na mama yake, Adeline Mukangemana, kwa, pamoja na makosa mengine,  kuchochea machafuko nchini humo.  Mashitaka hayo yalianza tena baada ya wanawake hao wawili kuachiwa kwa dhamana baada ya kukaa gerezai kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Katika kikao cha saa saba cha mahakama kilichofanyika Jumatano wiki hii, ambao wanasheria wa serikali walipitia video na vinasa sauti mbalimbali zikiwemo hati mbalimbali zilizochukuliwa nyumbani kwa washitakiwa, upande wa mashitaka ulisema ushahidi huo uliotolewa mahakamani unathibitisha nia yao ya kuchochea machafuko dhidi ya serikali.

Bi Rwigara, mkosoaji mkubwa wa serikali, anashitakiwa pia kwa kughushi hati za uchaguzi zilizomsababisha ashindwe kugombea urais mwaka 2017.

“Tunaomba Diane afungwe miaka 15 kwa kuchochea machafuko na miaka saba kwa kuwa na hati za kughushi,” walisema waendesha mashitaka mahakamani.

Hata hivyo, Rwigara (37) amekana madai ya kughushi akisema yalikuwa ni njama za kumzuia kupambana na Rais  Paul Kagame katika uchaguzi huo.

Pia ametetea msimamo wake wa kuikosoa serikali kuhusiana na haki za binadamu na alitoa wito kwa watu wa Rwanda “kutoogopa na kuisemea nchi yetu”.

Adeline Mukangemana ambaye ni mama yake Diaee Rwigara, akifikishwa mahakamani.

 

 

 

Comments are closed.