The House of Favourite Newspapers

Sabaya Awakana Wenzake Mahakamani

0

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuwa hawafahamu baadhi ya watuumiwa mwenzake katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake sita.

Akitoa Utetezi wake leo, Jumatano, Sabaya amedai kuwa mara yake ya kwanza kuwaona watu hao ni Juni 4, 2021 alipopandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ya uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Enock Togolon Mkeni Watson Mwahomange, na John Aweyo Odemba.

Vilevile amedai watuhumiwa wengine wawili Jackson Macha na Nathan Msuya waliletwa katika gereza la Kisongo Juni 21, 2021 ambapo nao walidai ni watuhumiwa wa kesi ile ile ya uhujumu Uchumi inayomkabili Sabaya.

Hata hivyo amebainisha kuwa mtuhumiwa Sylvester Nyegu alikuwa akimuona katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai kama mtumishi.

Leave A Reply