The House of Favourite Newspapers

Sabuni za King Limau na Marhaba Zaweka Rekodi Mitaani

0

KING Limau na Marhaba Soap ndiyo habari ya mjini! Hii ni kutokana na jinsi sabuni mpya za King Limau na Marhaba zinavyoendelea kuweka rekodi mitaani kufuatia uwezo wake mkubwa wa kuondoa madoa kwenye nguo, kuzitakatisha na kuzifanya nguo zako zing’are!

 

Kama ulikuwa unahangaishwa na madoa sugu kwenye nguo zako, mikono yako ilikuwa inachubuka kutokana na kutumia sabuni za kawaida na hupati harufu nzuri kwenye nguo zako baada ya kuzifua, basi hebu zijaribu King Limau na Marhaba uone ‘miujiza’ inayozidi kuwashangaza wengi.

 

Sabuni hizi mpya, zinazalishwa na Azania Group of Companies na ndani ya muda mfupi tangu ziingie mitaani, zimekuwa gumzo kubwa kutokana na uwezo wake mkubwa ukilingamisha na sabuni za kawaida.

Sifa yake kuwa ni kwamba zinang’arisha nguo na kuzifanya zionekane kwa rangi zake halisi, zina harufu nzuri, hazichubui mikono na zimetengenezwa kwa mchanganyiko maalum wenye uwezo wa kuondoa hata madoa sugu ambayo yameshindikana na sabuni nyingine.

 

“Hizi sabuni ni mpya kwetu sisi watumiaji, lakini baada ya kusikia sifa zake, nilipata shauku ya kwenda kujaribu ili nijionee mwenyewe.

“Tangu siku hiyo, sitaki tena kutumia sabuni nyingine zaidi ya King Limau na Marhaba kwa sababu zimenionesha maajabu,” Neema Salum, mama lishe anayefanya shughuli zake Tandale kwa Mtogole, alisema wakati akihojiwa kwenye promosheni ya sabuni hizo iliyofanyika wiki iliyopita kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

“Sisi mafundi wa magari kwenye gereji changamoto kubwa tunayoipata huwa ni nguo kuharibika na kupata madoa sugu kwa sababu ya kazi zetu, si unajua tena grisi, oili na mafuta mengine ya injini za magari yanaganda kwenye nguo!

 

“Lakini baada ya kutumia King Limau na Marhaba, hakika nimegundua kwamba kumbe inawezekana kuwa ‘smart’ hata ukiwa fundi gereji,” Juma Kigeu, fundi gereji maeneo ya Mabibo, naye alisema katika promosheni hiyo.

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, ulizia King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!

 

Kwa mawasiliano zaidi, wapigie kwa namba 0710 111 112 au watumie barua pepe kwa anuani ya email: sales@ azaniagroup.company. FAKI A. FAKI – +255 655 340 572 +255 713 340 572.

Stori: MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply