SADAKA HAIKOPESHWI

KAMA nakuona vile, unaringia gauni la dukani unasahau kama umevaa viatu vya mtumba, heeee heeeeiyaaa! Unalo mwaka huu shoga! Wanakwambia ukiona maharage yameiva jua mkaa umeteketea! Ulifi kiri mi wa kijijini nimekuja nanuka moshi kumbe wa mjini sitoki nje mpaka nijioshe! Halooo eeeehhhh! Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni, mbona roho itakutokaaa! Shoga baada ya udambwidambwi huo nikupe sasa kile

kilichonileta, tena usifi kiri ninacheka ukajua nina furaha shoga! Ifi ke mahali tusikaushane uzazi basi! Kila siku nikisema jambo lina maana yake ati! Leo nipo na nyie wanawake wenzangu, sijaja hata kuchamba bali kuelimishana tu maana mwaka ndiyo kama mnavyouona umeanza tena vibaya na mwezi ndiyo huo unakatika watu wakiwa hawana kitu mfukoni! Shoga siku hizi kila kona kwa siye wanawake tumegunduakitu kinaitwa mchezo, siyo

mchezo wa kitandani! Shuuuutuuuuu! Maana ulishaanza kutoa macho kama umegongesha gari la kuazima! Heee heeeeiyaaa, unalooooo eeehhh! Mwanamke wa siku hizi lazima ujue kujikunja bibi weee! Ukiachiwa kumi basi tano inaingia kwenye mchezo mwishoni mwa wiki au mwezi unavuta chako tena pesa ndefuuuu! Uongo? Hata kama utacheza mchezo wa shilingi elfu moja au mbili kwa siku au kwa wiki lakini mwisho wa siku utakuwa umeweka

sehemu ambayo itakufanya upate chochote! Najua wengine watajifanya kimbelembele kama fundi bomba wakati wamevaa dera inahu? Kama ulikuwa unajua kila usafi ri unahitaji konda basi umenoa, kwa taarifa yako bodaboda na bajaj wala hazihitaji konda! Ukiegemea kwenye mchezo wala hakuna cha kuwaza sijui kununua nguo za ndani, baba

watoto hajaacha hela unaanza kulaumu walaaaa! Shoga eeehhh, mchafu hachafuki na akichafuka basi alikuwa msafi huyo! Sadaka haikopeshwi kwa hiyo usije kuogopa kumuomba mumeo hela ya mchezo ili uwekeze na mwisho wa siku uweze kujiinua kiuchumi! Wanawake tuna ujanja mwingi, usiogope shoga kujibana ukapata japo ka elfu tano ka kuanzia mtaji wako wa mchezo tena nenda kaanze hata kwa elfu moja kwa wiki mwisho wa siku utanishukuru, upo nyonyo! Kwa leo nisiwe muongeaji saaana! Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine tamu zaidi! Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu!

Loading...

Toa comment