The House of Favourite Newspapers

Safari ya Okwi Simba, Dili Limeiva

0

MSHAMBULIAJI Emanuel Okwi ambaye ni rafiki mzuri wa kufumania nyavu, unaweza kusema kuwa rasmi kwa mara nyingine anaelekea kuwa mali ya Simba, hii ni baada ya kudaiwa kumalizana na klabu yake ya sasa ya Al Ittihad Alexandria ya nchini Misri.

 

Habari kutoka chanzo cha kuaminika cha ndani ya Klabu ya Simba, zimeliambia Championi Ijumaa kuwa, nguvu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, imetosha kukamilisha dili hilo la kumrejesha tena Okwi ndani ya kikosi hicho ili kuendeleza pacha yake matata aliyoiunda msimu wa 2018/19 akiwa na Meddie Kagere.

 

Wakati anaondoka Okwi alikuwa ametupia jumla ya mabao 15, huku Kagere akiwa na mabao 23, akiwa amefunga hat trick mbili katika Ligi Kuu Bara jambo ambalo limewafanya mabosi hao wa zamani kukubali arejee ili kuendeleza maisha ya kufunga mabao zaidi.

 

“Mpango mkubwa ni kurudisha ile pacha ya Okwi na Kagere ambaye amekuwa akifanya kazi kinyonge tofauti na msimu ule walipokuwa pamoja, ubora wao ulifanya wafunge jumla ya mabao 38 kati ya mabao 77 ambayo Simba ilifunga baada ya kucheza mechi 38.

 

“Tayari kila kitu kimekamilika, kinachosubiriwa kwa sasa ni kutambulishwa rasmi msimu ujao wa 2020/21 kwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenzake ambao tayari kimsingi ameshawaambia kwamba anarejea rasmi msimu ujao.

 

“Mo amefanikisha sehemu kubwa ya mipango ya Okwi kuondoka Misri huku jukumu la mwisho kabisa la kumalizana na klabu hiyo akimuachia Okwi mwenyewe ambaye naye anadaiwa kulikamilisha.

 

”Baada ya Simba kutangazwa kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo msimu wa 2019/20, Okwi alionekana akijibizana na wachezaji wenzake kwenye mitandao ikiwa ni pamoja na rafiki yake Clatous Chama ambaye alimwambia kuwa ataonana naye hivi karibuni.“Tutaonana nawe hivi karibuni kwa mara nyingine tena ninaamini katika hili na Mungu atusaidie,” aliandika Okwi

Leave A Reply