The House of Favourite Newspapers

Safisha Figo Kwa Kutumia Nanaa

0

LEO kwenye safu hii ya tiba kwa chakula tutaona jinsi Nanaa zinavyosaidia kusafisha figo kwani tatizo hili limekuwa kubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Nanaa inauzwa katika masoko mbalimbali nchini, ni mmea ambao unatumika sana kwenye mboga na matumizi mengine, kwa hapa kwenye safu yetu, tumeshawahi kuandika mara kadhaa kwani pia unatumika kwenye tiba ya chunusi.

Leo nakuelekeza jinsi ya kufanya ili ikutibu figo. Chukua fungu la majani ya mnanaa uoshe. Katakata vipande vidogo vidogo weka kwenye sufuria.

Mwagia maji safi na kisha chemsha kwa dakika kumi kisha acha yapoe. Baada ya hapo chuja vizuri hifadhi kwenye chupa safi kwenye friji ili iendelee kuwa ya baridi.

Kunywa glasi moja ya maji kila siku utaona mabadiliko, chumvi yote na uchafu mwingine uliokuwa umejikusanya utatolewa nje ya figo wakati wa kukojoa.

Utaweza kugundua mabadiliko ya mwili wako mwenyewe. Majani ya mnanaa yanajulikana kwa kiasi kikubwa kama tiba ya kusafisha figo na sehemu kubwa ya mmea huu ni asili.

Leave A Reply