The House of Favourite Newspapers

Safu ya Ulinzi Tatizo Mbeya Kwanza

0

KOCHA Msaidizi wa Mbeya Kwanza, Nizar Khalfan, amefunguka kuwa umakini mdogo kwenye safu yao ya ulinzi
imekuwa sababu kubwa
kwa kikosi chake kupata matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi Kuu Bara.

 


Mbeya Kwanza
imeruhusu mabao 16 katika michezo 14 waliyoshuka dimbani hadi sasa ikishika nafasi ya tatu kwa timu zilizoruhusu idadi kubwa ya mabao kwenye ligi msimu
 huu.


Akizungumza na
Spoti Xtra, kocha huyo alifunguka kwamba: “Tumeichukua timu ikiwa kwenye kipindi kigumu,
kuna changamoto nyingi
katika maeneo mengi kikosini, tumeruhusu mabao mengi mepesi ambayo yametokana na udhaifu kwenye eneo la ulinzi.

 

“Tunaendelea kulifanyia kazi ili tuweze kuwa na timu imara kwani hatupo katika nafasi nzuri kwenye msimamo, hivyo tunahitaji kupambana kujiondoa huko na njia pekee ni kupata matokeo mazuri kwenyemechi zote zilizosalia.”

 


Kabla ya mechi za jana,
Mbeya Kwanza ilikuwainashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi
Kuu Bara ikiwa na pointi
13, imeshinda mechi mbili, sare saba na kupoteza tano.

STORI NA HUSSEIN MSOLEKA | SPOTI XTRA

RAIS SAMIA ATEMA CHECHE: “MKUU WA MKOA ni KAMA UMEOTA, ILIKUWA NIKUFYATUE LEO HAPA HAPA”

Leave A Reply