The House of Favourite Newspapers

Sajenti Aeleza Alivyoachiwa Kovu Na Mtoto Patrick

STAA wa filamu kutoka Bongo Movie, Husna Idd ‘Sajenti’ ameeleza machungu yake kwa aliyekuwa mtoto wa msanii mwenzake ambaye ni rafiki yake wa karibu, Rose Alphonce, marehemu Patrick na kusema kuwa amemuachia kovu kubwa.

 

Akizungumza na Ijumaa, Sajenti alisema kuwa, Patrick enzi za uhai wake alikuwa ni rafiki mkubwa wa watoto wake na walikuwa wamezoeana sana hivyo alivyopata taarifa za kifo chake aliumia na hakuamini kwa kile kilichotokea kwa sababu ni mtoto aliyekuwa akimpenda na hata watoto wake walimzoea.

 

“Nilivyopata taarifa za kifo cha Patrick kwa kweli niliumia sana, nilijaribu kujiangalia nilivyomzoea nikajikuta huzuni kubwa ikinitawala, sikuweza kulala kabisa, kutwa nikilia kwa uchungu kwa sababu tu nilivyokuwa nimemzoea Patrick na hata watoto wangu,” alisema Sajenti.

Akiendelea kuzungumza na Ijumaa Sajenti, alisema kuwa Patrick amemuachia kovu kubwa ambalo haliwezi kupona milele anachofanya sasa hivi ni kumuomba Mungu, ampe subira mpaka atakapompokea mtoto huyo (jana au leo).

 

“ Hapa namuomba Mungu tu, anipe ujasiri niweze kupata nguvu ya kupokea mwili wake niamini kabisa hayupo nasi maana nina kovu kubwa ambalo haliwezi kukauka kwenye moyo wangu,” alisema Sajenti kwa masikitiko.

 

Mtoto Patrick alifariki Jumanne iliyopita jijini Nairobi alipokuwa amepelekwa na mama yake huyo kwa ajili ya kufanyiwa matatibu baada ya kugundulika kuwa na uvimbe kwenye ubongo.

 STORI: IMELDA MTEMA, IJUMAA

Comments are closed.