The House of Favourite Newspapers

Sakata la Deni la Taifa “Tukope Tusikope”?

0

MGONGANO wa mawazo kuhusu nchi kukopa au kutokukopa uliojitokeza kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na Rais Samia Suluhu Hassan umezidi kushika kasi.

 

Msimamo wa spika aliotoa ni kwamba nchi kuendelea kukopakopa kuna siku “itauzwa” na hivyo kutaka mpango huo usitishwe na taifa liweze kujitegemea.

 

Rais Samia alipoibuka wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR kutoka Makutupora hadi Tabora alisema kwa msisitizo kuwa “Tutakopa”.

 

Mitandaoni na kwenye vijiwe mbalimbali mjini wengi wanamuunga mkono Rais Samia kwa kusema “Tukope” ambapo watu wengine hasa makada wa upinzani nao wameunga mkono hoja ya kukopa mfano ni Godbess Lema.

 

Lakini kwa upande mwingine wengine wamemuunga mkono spika Ndugai kwa kusema madeni ni mzigo kwa taifa hasa linapokuja suala la matumizi mabaya ya mikopo hiyo.

 

Kusema kweli kauli hizi kinzani zinaonekana kama kuchagua kati ya MVUA na JUA. Hebu na wewe jitutumue kujibu kwa ufahamu wako “TUKOPE” “TUSIKOPE?”
Na @manyota_rich 

Leave A Reply