The House of Favourite Newspapers

Sakata La Fei Toto Lamuibua Kigogo Serikalini, Afunguka Mazito Kumaliza Suala Hilo

0
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay.

KUFUATIA sintofahamu iliyopo kati ya uongozi wa Yanga na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ limemuibua Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay kwa kutaka busara itumike kumaliza suala hilo.

Mayay ametoa kauli hiyo kufuatia sakata la muda mrefu kati ya Fei Toto na mabosi wake hali iliyopelekea kuwa nje ya timu hiyo huku akiwa ametangaza kuvunja mkataba na Yanga kabla ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuweka wazi kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga.

Kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’

Akizungumza na Spoti Xtra, Mayay alisema kuwa inahitajika busara kubwa kutoka pande zote mbili ili kulimaliza sakata hilo kutokana na kila upande kupata athari zake ambazo zinahitaji kumalizwa haraka.

“Nadhani jambo kubwa ni wao kutumia busara  upande wa Yanga na hata upande wa Fei, ili kumaliza hili sababu kinachotokea kwa sasa ni athari ambazo kila upande umekuwa ukizipata kutokana na kutofikia hatua nzuri kwao kulimaliza  hili.

“Kila mtu bado anahitaji kitu kutoka kwa mwenzake kwa sababu Yanga wao watakuwa waathirika kibiashara kwa kuwa wanamkosa mchezaji, lakini hata mchezaji atakuwa anapata wakati mgumu kutokana na kukosa stahiki zake lakini hata kipaji chake kwa kuwa muda mwingi amekuwa nje ya timu, hivyo wanayo nafasi wenyewe kutumia busara kumaliza jambo hili,” alisema Mayay.

TUNDU LISSU AIBUA MAPYA – ”VYUMA VIMEKAZA, CCM NILIACHANA NAYO NILIPOJIUNGA CHUO KIKUU”

Leave A Reply