The House of Favourite Newspapers

Sakata la Kijana Aliyeuawa kanisani, ACT Waicharukia Polisi! – VIDEO

Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Singida kuhusu uchunguzi wa Tukio la mauaji linalodaiwa kutekelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Pius Luhende kanisa la Adventisti mkoani humo.

Akizungumza na waandishi katika ofisi za makao makuu ya chama hicho yaliyopo kijitonyama jijini Dar es salaam Katibu wa Itikadi Mawasiliano na Uenezi Ado Shaibu amesema chama hicho kimeshtushwa na taarifa kutoka katika jeshi la polisi mkoani humo iliyonukuliwa na vyomba vya habari.

Aidha Shaibu amesema kwa mujibu wa Baba wa Marehemu na waumini wa kanisa hilo wamesema aliyemfyatulia risasi marehemu ni Mkurugenzi wa Itigi.

Shaibu amesema chama cha ACT kinalaani tukio hilo la kinyama lililofanyika kwenye nyumba ya Ibadan a kutaka haki itendeke bila kuangalia cheo cha mtu na mahusiano yake kwa Serikali. February 2 mwaka huu inadaiwa Mfanyabiashara Isaka Petro aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ibadani katika kanisa la Kiadventisti Itigi mkoani Singida na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi Pius Luhende

Comments are closed.