The House of Favourite Newspapers

SAKATA LA WATOTO: MAKONDA AKANUSHA ORODHA YA VIGOGO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikiwa na orodha ya majina ya watu akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa na baadhi ya wabunge kuwa wameitwa ofisini kwake kwa madai ya kutekeleza watoto wao.

 

Makonda amesema kuwa, taarifa hiyo ni propaganda zenye lengo la kupotosha na kupaka matope zoezi la kuwasaidia akina mama wanyonge waliotelekezwa.

 

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwa zoezi analoliendesha la kuwasaidia kina mama na watoto waliotelekezwa halitamuonea mtu yeyote  na halitamuogopa mtu yeyote atakayethibitika kutotoa matunzo kwa mtoto wake kwa mujibu wa sheria.

 

Hata hivyo amesema kuwa familia 170 ambazo zilikwenda jana ofisini kwake waliweza kuelewana namna ya kulea watoto wao na kusema zoezi linakwenda vizuri kama ambavyo lilikusudiwa na kudai kuanzia Jumatatu sasa wataanza kuitwa wakina baba.

 

=========================

 

TAARIFA YA UZUSHI ILIYOKUWA INASAMBAZWA

MAKONDA ATAJA WATU 10 KURIPOTI OFISINI KWAKE IJUMAA.

Na Mwandishi wetu,

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda ametaja orodha ya watu kumi ambao ameagiza wafike ofisini kwake siku ya ijumaa tarehe 13 April kuanzia saa 2 asubuhi.

Katika taarifa aliyoitoa leo mchana Makonda hajaeleza sababu ya kuwaita watu hao lakini inadhaniwa ni suala la madai ya kutelekeza watoto. Watu hao ambao Makonda anadai kuwaandikia barua ni pamoja na:

1. Mhe.Edward lowassa (waziri Mkuu mstaafu)

2. Mhe.Peter msigwa (mbunge Iringa mjini)

3. Mhe.Godbless lema (mbunge Arusha mjini)

4. Mhe.Hussein Bashe (mbunge Nzega mjini)

5. Mhe.Peter Lijualikali (mbunge Kilombero)

6. Mhe.Freeman mbowe (mbunge Hai)

7. Mchungaji Daniel Joshua (True Life Ministry)

8. Padri Baptiste Mapunda (RC)

9. Baba Askofu Josephat Gwajima (Ufufuo na uzima)

10. Bwana Dismas Lyassa (mwandishi wa habari)

Comments are closed.