The House of Favourite Newspapers

Salah, Mane, Ronaldo, Messi, Wengine 26 Kuwania 2018 Ballon d’Or

Shirikisho la Soka la Ufaransa limetoa majina 30 ya wachezaji soka watakaowania tuzo ya Ballon d’Or  kwa mwaka  2018.  Wachezaji wawili wa Afrika katika orodha hiyo ni Mohamed Salah wa Misri na Sadio Mane wa Senegal, wote wakichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza.

Wachezaji wengine maarufu ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar Jr., Paul Pogba, Kylian Mbappe, Luka Modric, N’golo Kante, Luis Suarez.

Makipa ni pamoja na mchezaji wa Ubelgiji na Real Madrid, Thibaut Courtois, mchezaji wa Ufaransa na klabu ya Tottenham, Hugo Lloris, mchezaji wa Brazil na Liverpool, Alisson  na mchezaji wa Slovenia na  Atletico Madrid, Jan Oblak.

Ballon d’Or (Mpira wa Dhahabu) imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1956, na 2010, iliunganishwa na ile ya shirikisho la soka duniani ya FIFA’s The Best Award  na kuwa FIFA Ballon d’Or. Hii iliendelea hivyo hadi 2016.

Cristiano Ronaldo ameshinda zawadi hizo mbili zilizopita za Ballon d’Or. Utoaji wa zawadi unategemewa kufanyika Desemba 3 jijini Paris, Ufaransa.

Comments are closed.