The House of Favourite Newspapers

Salamu za Rais Magufuli, RC Makonda Msiba wa Isaac Gamba – Video

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW), Isaac Muyenjwa Gamba umeagwa leo Jumatatu, katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye utapelekwa airport tayari kwa safari kuelekea kwao Bunda kupitia Mwanza kwa ajili ya maziko.

 

Miongoni mwa Viongozi wa serikali waliofika katika kuaga mwili huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ambaye alipata fursa ya kutoa salam za rambirambi alizoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

 

“Nilipopata taarifa za msiba nilisikitika sana, Isaac ndiye alinifanya nijulikana kule (Ujerumani), kila tukio lilipokuwa likitokea Dar es salaam alikuwa akiwaambia wenzake ‘Mtafuteni Kamanda Makonda tujue ukweli’, lakini kwa taarifa zilizopo siyo ugonjwa ule tuliyokuwa tukiuhisi, majira na nyakati za Mungu zilivyowadia akamchukua.

 

“Niwape pole wanahabari wote kwa msiba huu, niwaombe muendeleze umoja wa wanahabari ambao ndiyo unaweza kulitunza taifa letu. Tuwasaidie vijana wengine wenye uwezo, Isaac hakufanya haya kwa faida yake pekee, lakini alisaidia na vijana wengine kuinua vipaji vyao kwa manufaa ya Taifa zima,” alisema Makonda.

 

Naye Gerson Msigwa akapata fursa ya kutoa salam za rambirambi kwa niaba ya Rais Magufuli;

 

“Kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, niwape pole wote mliofika hapa kumuaga ndugu yetu Isaac. Rais anasema angetamani leo awe nasi hapa kumuaga ndugu yetu, lakini majukumu yamembana, Rais anawapa pole sana na kwa sasa kikubwa zaidi tumuombee apumzike mahali pema,” alisema Msigwa.

 

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.