The House of Favourite Newspapers

Saleh Ally: Injinia Hersi Hakustahili Kugombea Nafasi ya Urais wa Yanga(PICHA+VIDEO)

0
Saleh Ally ‘Jembe’ Mchambuzi wa soka

MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally Maarufu kama ‘Jembe’ ametoa maoni yake juu ya nafasi ya Injinia Hersi Said kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais wa Klabu ya Yanga.

Injinia Hersi Said mgombea Urais wa Klabu ya Yanga

Jembe amesema kuwa kwa mtazamo wake Injinia Hersi hakuwa mtu sahihi kugombea nafasi hiyo kutokana na kile alichokiita mgongano wa masilahi (Conflict of Interest) ambapo amebainisha kuwa kazi ya Urais ndani ya klabu ya Yanga haina malipo au mshahara na Hersi ni mfanyakazi au mwajiriwa wa Mdhamini wa Yanga ambaye ni GSM.

Jembe amesema Injinia Hersi Hakustahili kugombea nafasi ya Urais wa Yanga

Kwa mtazamo wa Jembe ni kwamba itakuwa vigumu sana kwa Injini Hersi Said kupambania masilahi ya klabu hasa pale inapokuja mtazamo tofauti ya mlengo wa klabu na mlengo wa Mdhamini ambaye ndiye mwajiri wake na ndiye anayemlipa mshahara.

 

Kwa upande mwingine Jembe amesema kwa kuwa tayari nafasi ya mgombea wa urais amebaki pekeyake hivyo hakuna namna tena Zaidi ya kushuhudia Injinia Hersi akienda kuchukua kiti cha Urais wa Yanga, ingawa ametoa angalizo kwamba kwa nafasi hiyo lazima atapokea changamoto kubwa na lazima awe tayari kukubali kukosolewa.

Leave A Reply