The House of Favourite Newspapers

Saleh Ally: Sakho ni Mchezaji Halali wa Simba, Hayupo Pale kwa Mkopo

0
Mchambuzi wa Soka Saleh Ally ‘Jembe’

MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally Maarufu kama ‘Jembe’ amesema Mchezaji wa Simba SC Pape Ousmane Sakho ni mchezaji halali wa klabu hiyo na kwamba atendelea kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

 

Mchambuzi huyo ameyasema hayo wakati wa kipindi cha Krosi dongo kinachorushwa na Global Radio na Global TV ambapo amebainisha kuwa Sakho hayupo Simba kwa mkopo kama inavyosemekana kwenye mitandao ya kijamii.

“Mi sidhani kama Simba watakuwa tayari kumuachia Sakho, kabla hatujawajudge wachezaji wapya wanaokuja Simba kwa sasa Sakho ndiyo Staa na hayupo Simba kwa mkopo.” alisema Jembe

Pape Ousmane Sakho, mchezaji wa Simba

Kumekuwa na taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa Sakho alisajiliwa na Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja ili kupata fursa ya kuonekana katika michezo ya kimataifa na baada ya hapo atatimka na kwenda kucheza soka kwenye timu nyingine tofauti na Simba SC.

 

Pape Sakho amekuwa na kiwango cha hali juu hasa katika michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo klabu yake ilitolewa katika hatua ya robo fainali na Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

Leave A Reply