The House of Favourite Newspapers

Saleh Jembe: Yanga Inatakiwa Kujipanga Kisawasawa Kuwakabili Al Hilal

0
Saleh Ally ‘Jembe’

MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally maarufu kama Jembe amesema kuwa klabu ya Yanga inapaswa kujipanga kisawasawa ili kuweza kuikabili klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan katika hatua ya raundi ya kwanza kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

 

Jembe ameyasema hayo katika kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na studio za Global TV na 255global radio ambapo amebainisha kuwa kwa ubora na ukubwa wa Al Hilal katika soka la ukanda wa CECAFA ni wazi Yanga inatakiwa kujidhatiti vya kutosha kama inataka kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo.

“Mimi naamini Yanga wakijiandaa na wakacheza kwelikweli na wakweka kwenye kichwa chao kwamba mechi ya kwanza ndiyo mwamuzi wao basi mi naamini wanaweza wakafanya vizuri.” amesema Jembe.

Yanga inatarajiwa kuanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Al Hilal katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Mchezo wa awali kati ya Yanga na Al Hilal unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kati ya Oktoba 7-9 na marudio itakuwa ni kati ya Oktoba 14-16 mwaka huu.

 

Al Hilal imefanikiwa kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili mnamo mwaka 1987 pamoja na mwaka 1992 ambazo kwa mara zote hizo ilipoteza kwa Al Ahly ya Misri pamoja na Wydad Casablanca ya nchini Morocco.

 

Leave A Reply