The House of Favourite Newspapers

Salum Mkemi Atangaza Kujiuzulu Uongozi Yanga

Mjumbe wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi.

 

MJUMBE wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amejiuzulu nafasi uongozi ndani ya klabu hiyo kuanzia leo. Maneno hayo ameyasema kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya timu ya Yanga kuaga kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup inayoendelea nchini Kenya baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Kakamega Boys kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Ifraha nchini Kenya.

Haya ndo maneno aliyoyasema kupitia akaunti yake ya Instagram

Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi 
Kwa Hakika Tumepata Aibu Kubwa Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili 
Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza 
Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza. 
Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi 
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club “YANGA ” kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.
Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika 
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu 
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu 
SALUM MKEMI
NIMENG’ATUKA

Comments are closed.