The House of Favourite Newspapers

Samaki wa Kukaanga na Ndizi Mzuzu

LEO tunaa-ngalia jinsi ya kupika ndizi mzuzu za kukaanga na samaki.

Maandalizi:

-Samaki sato vipande utakavyo.

-Ndizi mzuzu zikatekate.

-Mafuta ya kupikia.

-Vitunguu na nyanya.

Viungo:

Kitunguu swaumu, pilipili manga na limao.

Chukua samaki, mpake viungo nilivyoku-andikia hapo, hapa kwenye suala la viungo kila mmoja anavyo vyake anavyo-vipenda, sasa ni wewe kuchagua.

Jinsi ya kupika:

Ukishapaka samaki wako viungo, mkaange kisha weka pembeni.

Chukua ndizi mzuzu nazo zikaange kisha ziweke pembeni.

Baada ya hapo, panga kwenye sahani kwa ajili ya kula.

Ukimaliza, unga sosi ya nyanya na kitunguu kisha weka pembeni kwenye sahani yako unayolia, chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Gladness Mallya

Comments are closed.