The House of Favourite Newspapers

SAMATTA ALIVYOWATEKA WAZUNGU

Mbwana Samatta

MBWANA Samatta amezidi kung’ara kwenye vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja. Samatta ambaye anaichezea KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji, ndiye kinara wa wafungaji wa ligi hiyo akiwa ametupia mabao 15 katika michezo 20 aliyocheza.

 

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC na TP Mazembe, sasa thamani yake inatajwa kuwa zaidi ya Sh bil 17 ambapo alitua Genk kwa Bil 1.3 tu mwaka 2016.

 

Kazi ya staa huyo mwenye urefu wa futi tano na inchi 11, imemfanya ahusishwe kutakiwa na klabu mbalimbali ikiwemo Everton ya England na nyingine kadhaa. Sasa hebu tucheki baadhi ya timu ambazo zinatajwa kumfukuzia.

 

CARDIFF CITY Cardiff City inayoshiriki Ligi Kuu ya England inapambana kusaka saini ya mshambuliaji ili iweze kuongeza kasi zaidi kwenye ligi.

Timu hiyo iliyopo Wales, imekuwa timu ya hivi karibuni kudaiwa kumtaka Samatta na inadaiwa kuwa ipo tayari kutoa pauni milioni 12 ili iinase saini ya Mtanzania huyu. Hata hivyo, dili la Samatta linaweza kutiki ikiwa Cardiff itashindwa kumsaini mshambuliaji chaguo la kwanza, Emiliano Sala ambaye amefunga mabao 12 katika mechi 19 za Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1, akiwa na kikosi cha Nantes.

 

EVERTON

Klabu hii ambayo pia aliichezea Wayne Rooney, inatajwa kuwa kwenye mipango ya kutaka kumsaini Samatta awe mbadala wa Oumar Niasse ambaye inaripotiwa ana mpango wa kuondoka Goodison Park, Januari hii.

 

Tangu ilivyomuuza Romelu Lukaku kwenda Manchester United, Everton imekuwa ikikosa mtu sahihi wa kusimama mbele na inaona kama Samatta ni suluhisho.

 

WEST HAM

Gazeti la Daily Mirror la Oktoba 6, mwaka jana katika ukurasa wa 63, liliripoti kuwa West Ham ilikuwa ikimfukuzia mshambuliaji huyo Mtanzania ili imsajili kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji asaidiane na Marko Arnautovic na Andy Carroll ambaye amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

 

FENERBAHCE Hivi karibuni, magazeti matatu ya Uturuki yaliripoti kuwa Kocha wa Fenerbahce, Ersun Yanal alipendekeza Samatta asajiliwe kikosini humo haraka. Kocha huyo alifikia uamuzi huo kutokana na nyota wake Andrew Ayew wa Ghana kushindwa kung’ara kama Samatta ambaye kwa sasa ana mabao 15.

 

LEVANTE

Kama dili lingetiki au litatiki basi Samatta atakuwa akipambana na Lionel Messi wa Barcelona na beki wa Madrid, Sergio Ramos yeye akiwa na uzi wa Levante ambao walikuwa wakimtaka tangu Julai, mwaka jana. Kiwango alichoonyesha kwenye michuano ya Europa msimu uliopita, ndiyo ilikuwa mwanga zaidi kwake kujitangaza ndiyo maana klabu kubwa zimekuwa zikimfukuzia.

 

CSKA MOSCOW

Klabu hii kutoka Urusi nayo ni sehemu ya timu kibao zilizotajwa kumuwania Samatta ili akaongoze safu ya ushambuliaji kwenye kikosi chao kinashoriki ligi kuu ya nchini humo.

 

KLABU ZINGINE

Zipo klabu nyingi kutoka Ulaya ambazo zimekuwa zikitajwa kumtaka mshambuliaji huyu, baadhi ni zile za kutoka Premier League ambazo Brighton, Bournemouth na Burnley.

Comments are closed.