The House of Favourite Newspapers

Samatta: Watanzania Msiwatukane Wachezaji wa Aston Villa, Sifurahishwi

0

NAHODHA  wa timu ya taifa (Taifa Stars) anayechezea Klabu ya Aston Villa ya Uingereza, Mbwana Samatta,  ameomba Watanzania kuacha kutoa maneno ya kashfa kwenye akaunti za Aston Villa na za wachezaji wa timu hiyo.

 

Baadhi ya mashabiki toka Tanzania wamekuea wakifanya kitendo hicho ambacho amesema hakimfurahishi.

 

Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vzr ktk timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika ac/ za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi,” amesema Samatta.

Leave A Reply