The House of Favourite Newspapers

Sanamu ya Taswira ya Ngono Yamfadhaisha Mhojiwa kwenye TV

0

MWANAMKE mmoja, Yvette Amos, wa Uingereza, alipata mfadhaiko mkubwa baada ya kuhojiwa katika kipindi cha BBC Wales Today wakati nyumba yake katika mashubaka ya vitabu vyake kulikuwa kuna sanamu iliyokuwa ikionyesha taswira ya mambo yanayohusiana na ngono.

 

Mwanamke huyo alitokea katika kipindi hicho jana jioni (Jumanne) ili kujadili masuala ya ukosefu wa ajira wakati wa janga la ugonjwa wa Covid-19.

 

Sanamu hiyo ilionekana na watu waliofuatilia kipindi hicho ikiwa imewekwa nyuma yake na kuwaacha wakiwa wamepigwa butwaa.

 

Mwandishi mmoja wa habari alitoa tahadhari na kusema ni vyema wahojiwa wakawa wnatazama kwanza nyuma yao kabla ya kuanza kuhojiwa.

 

Watumiaji wa Twitter waliliita tukio hilo la kuchekesha na lilivuma katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengine walisema hicho kilikuwa ni kichekesho tu na wengine wakasema kuna mtu alimtegeshea mwanamke huyo sanamu hiyo bila yeye kujua.

Leave A Reply