The House of Favourite Newspapers

Sanches Afunguka Mkataba wa Arsenal

LONDON | England |CHAMPIONI IJUMAA

WAKATI sakata la uhamisho wake kuwa anaweza kuondoka Arsenal likiendelea, mshambuliaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez amefunguka juu ya muelekeo wake kisoka. Sanchez amesema kuwa ana furaha kuwa klabuni hapo na anaimani kuwa atamaliza mkataba wake uliosalia miezi 15 hapohapo lakini ametoa angalizo.

Staa huyo wa Chile amesema kuwa anataka kucheza katika timu ambayo inakuwa na moyo wa ushindi. Sanchez ambaye inaelezwa anawaniwa na Chelsea, amekuwa akikwaruzana na kocha wake na wachezaji wenzake kutokana na mwelekeo mbaya wa timu hiyo katika siku za hivi karibuni kiasi cha kuelezwa kuwa hana furaha.

“Nina furaha kuwa Arsenal, naamini nitamaliza mkataba wangu hapo, nataka kuendelea kubaki kwenye mji huo (London) lakini hilo litawezekana katika timu ambayo ina moyo wa kushinda.

“Nina miaka 28, bado nina mengi ya kufanya mbele yangu, mimi ni mchezaji ambaye nimekuwa nikijichunga sana,” alisema.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.