SANCHI AANIKA SABABU YA KUPIGA ZA UTUPU

Jane Ramoy ‘Sanchi’

MWANAMITINDO maarufu Bongo na Afrika Mashariki, Jane Ramoy ‘Sanchi’ amesema kuwa picha zozote zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha yuko wazi sehemu kubwa ya mwili wake si kwamba anazipiga ili apate fedha kutoka kwa wanaume watakaomtongoza bali sababu kubwa ni kwamba yeye ndivyo anavyopenda. 

 

Akizungumza na Amani, Sanchi alisema kuwa kuna watu wengi wanafikiri akipiga picha vile labda anatafuta wanaume ili wampatie fedha, kitu ambacho sio cha kweli kwani yeye ana mtu wake na anamuelewa anachofanya.

 

“Watu wengi sana wananifikiria tofauti labda napiga picha kujiuza au kuwateka wanaume kumbe mimi nafanya kitu ambacho nakipenda toka moyoni na si vinginevyo,” alisema Sanchi ambaye mara kwa mara amekuwa akizungumzwa kwa kupiga picha za utupu na watu kuhoji kwa nini Baraza la Sanaa (Basata) hawamshughulikii. Hata hivyo, Basata wameshindwa kumshughulikia kwa kuwa hajajisajili katika baraza hilo.

Loading...

Toa comment