MAN U YAISHANGAZA JUVE, YAIGONGA 2-1

TIMU ya Manchester United ya Uingereza imeishangaza klabu bingwa ya Italia, Juventus,  kwa kuipiga mabao mawili katika tano za mwisho za hatua za mitoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Juan Mata alifunga bao la kusawazisha alipopiga mpira wa adhabu ukaenda moja kwa moja golini, na baadaye mkwaju uliopigwa na Ashley Young ulitumbukizwa golini na mlinzi wa Juventus, Alex Sandro.

Cristiano Ronaldo alikuwa amefunga bao la kuongoza kwa timu hiyo iliyokuwa ikicheza nyumbani dhidi ya klabu aliyowahi kuichezea.

Ronaldo alipokea pasi ndefu kutoka kwa Leonardo Bonucci kabla ya kuupiga na kumpita kipa  David De Gea wa Man U, likiwa bao lake la kwanza katika mashindano hayo tangu alipojiunga na klabu hiyo.

 

Wachezaji wa Juventus walipiga mashuti yaliyogonga miamba mara mbili kutoka kwa  Sami Khedira na Paulo Dybala katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Timu hiyo ya Jose Mourinho haikuonyesha tishio lolote hadi Mata alipoingia na kuukwamisha mpira wavuni dhidi ya kipa Wojciech Szczesny katika dakika ya  86.

Dakika tatu baadaye mpira wa adhabu uliopigwa na Young ‘ulisaidiwa’  kwa kutumbukizwa wavuni na mlinzi wa Juventus,  Sandro.

Mabao hao ya Man yanawaweka katika nafasi ya pili katika Kundi H.

 

 

 

 

Vidokezo:

  • Juventus ilipoteza mchezo wa nyumbani katika kundi la Ligi ya Mabingwa mara ya kwanza Desemba 2009 ilipopigwa na  Bayern Munich baada ya kucheza mechi 19 bila kufungwa.
  • M. United wameshinda mechi nyingi za ugenini — mechi tatu — katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus kuliko timu yoyote katika mashindano hayo.
  • United wameibuka na kushinda mchezo wa ligi hiyo kwa magoli mawili katika dakika tano za mwisho kwa mara ya kwanza tangu  1999 walipocheza dhidi ya Bayern Munich.
  • Juan Mata alifunga bao lake la kwanza katika ligi hiyo tangu alipofunga dhidi ya Wolfsburg mnamo Septemba 2015.
  • Manchester United imeshinda mechi 3 mfululizo bila uwepo wa Romelu Lukaku.

Juventus XI: Szczesny; De Sciglio, Chiellini, Bonucci, Alex Sandro; Khedira, Pjanic, Bentancur; Dybala, Cristiano Ronaldo, Cuadrado.

Manchester United: De Gea; Young, Smalling, Lindelöf, Shaw; Matic, Pogba, Herrera; Lingard, Alexis, Martial.

 

Toa comment