The House of Favourite Newspapers

SANCHI AVUTIWA NA UHUSIANO WA MONDI NA TANASHA

Jane Ramoy ‘Sanchi’

MWANAMITINDO Jane Ramoy ‘Sanchi’ ameeleza kuwa anavutiwa sana na uhusiano wa kimapenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Sanchi’ na Tanasha Donna huku akiwaombea wafike mbali.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Sanchi alisema anafikia hatua ya kusema hayo baada ya kuwepo kwa manenomaneno kwamba yeye ni kati ya watu wanaoiponda kapo hiyo bila kujua kuwa yeye ni shabiki namba moja wa wawili hao.

“Kuna maneno watu wanaweza kusambaza yasio na kichwa wala miguu lakini ukweli ni kwamba mimi ni shabiki namba moja wa uhusiano wao na ninawaombea kwa Mungu wafike mbali zaidi. “Ninavyoona watadumu muda mrefu tofauti na uhusiano mwingine kwani Diamond ameshapitia mambo mengi na inaonekana anampenda Tanasha kutoka ndani ya moyo wake,” alisema Sanchi.

Comments are closed.