The House of Favourite Newspapers

Sanchi: Sijutii Kubadili Dini

0

MREMBO ambaye alipata umaarufu kutokana na kujaaliwa umbo matata la kuvutia, Surraiya Rimoy ‘Sanchi’ anasema kuwa, hajutii hata kidogo kitendo chake cha kubadilisha dini kutoka kuwa Mkristo na kuwa Muislam kwani imemfanya awe anajua kusali na jinsi ya kujisitiri.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Sanchi anasema kuwa, kila mwanadamu ana nguvu yake ya kumfanya abadilike na kuwa tofauti kabisa na huko nyuma na ndivyo iliyokuwa kwa upande wake.

Sanchi anawashauri wasichana wengine wajue jinsi ya kujirudisha na kuwa tofauti kabisa kwa mema na mtazamo tofauti kwa watu.

 

“Kuna watu wanafikiri najutia uamuzi niliofanya, hapana, sijutii kubadili dini, nafurahia sana kitu nilichoamua kwani ni kikubwa kwenye maisha yangu sijui nisemaje, lakini ukweli kabisa nimejua kusali, nimejua kuvaa mavazi mazuri na ya heshima na hicho ndicho kikubwa kwangu,” anasema Sanchi ambaye kwa sasa amekuwa akijistiri mno tofauti na alivyokuwa zamani.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

RUSSIA vs UKRAINE: CHANZO KAMILI CHA UGOMVI WAO NI HIKI, WALIANZA KAMA UTANI, SASA WANATIKISA DUNIA!

Leave A Reply