The House of Favourite Newspapers

Sandakalawe Ya Harmonize Yaondolewa Youtube

0

WIMBO wa msanii wa muziki wa Bongo Flava, Harmonize uitwao Sandakalawe Juni 28, 2021 umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na masuala ya hakimiliki.

 

Taarifa za mtandao huo zimeleeza kuwa kampuni ya usambazaji muziki ‘Empire’ imelalamika kuwa wimbo huo umechukua baadhi ya vionjo kutoka kwao.

 

Kutokana na hilo, wimbo huo umezuiwa hadi pale pande hizo mbili zitakapokaa na kukubalia. Hivyo kwa sasa mashabiki wa Harmonize nchini hawataweza kuusikiliza wimbo huo kupitia YouTube.

Leave A Reply