Sanjay Mkongwe wa Filamu za Kihindi Atua Bongo

Mbunge Gulamali (kulia) akiwa na Sanjay.

 

Msanii mkongwe wa filamu kutoka India (Bollywood), Sanjay Balraj Dutt ametua nchini hivi karibuni na kupokelewa na Mbunge wa Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Seif Khamis Gulamali (CCM) tayari kwa ziara yake ya kutembelea vivutio vya utalii.

Imeelezwa kuwa ameanza kwa kutembelea na kupumzika katika mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.

 

Wakiteta jambo.

 

Sanjay ambaye wazazi wake pia walikuwa nguli wa Bollywood, Sunil Dutt na Nargis Dutt, alizaliwa Julai 29 mwaka 1959. Mbali na uigizaji pia ni producer mzuri wa filamu hizo.

Sanjay amewahi kucheza filamu zaidi ya 100 tangu mwaka 1981 alipoanza uigizaji rasmi, hasa akibeba uhusika wa kimapenzi na uchekeshaji (komedi).

Sanjay akipokelewa na Gulaman.

 

Katika miaka 35 ya uigizaji, Sanjay amewahi kutwaa tuzo lukuki zikiwemo  Filmfare Awards (mbili), IIFA Awards, Bollywood Movie Awards (mbili), Screen Awards (tatu), Stardust Awards (tatu), Global Indian Film Award (moja) na Bengal Film Journalist’s Association Award (moja). Filamu zake nne zilishinda vipengele mbalimbali vya National Film Awards.

Loading...

Toa comment