The House of Favourite Newspapers

‘Sapraizi’ kwa wanandoa iwe tuzo kila mwaka

0

couples_gifts-680x430Asalam alaikum wapenzi wasomaji wa safu hii maridhawa, leo nina furaha kwa ajili ya mada hii niliyokuja nayo hivyo nianze kwa kuwaombea dua wasiokuwa na ndoa wapate ndoa na walio kwenye ndoa, ndoa zao zidumu ishallah.

Leo nimeamua kuwaletea mada hii ya kupeana tuzo kwa wanandoa kwani wanandoa wengi tunasahau tulipotoka na kubeba mabaya ya wenzetu tu bila kukumbuka mazuri tuliyofanya pamoja.

Kwa kuanzia hapo nikukumbushe tu wewe uliye kwenye ndoa yako kukumbuka kumpa sapraizi mume wako au mke wako ikiwa kama tuzo kwa mazuri aliyokufanyia.
Tusiishie kusema asante tu hiyo haitoshi tuandae na kitu cha kumshtukiza mwezi wako ili kuliboresha penzi.

Jinsi ya kumpa tuzo mume/mke wako
Bila shaka watu wengi wanajua sapraizi, kwani si kitu kigeni kwa wapenzi lakini kwa wanandoa huwa ni mara chache sana mtu akishamuoa mwanamke au mwanamke akishapata mume huwa ndiyo anaona amemaliza siyo rahisi hata kumpa zawadi mwenzake.

Mke wako au mume mshtukize kwa kumuandalia vitu ambavyo si vya kawaida, unaweza kuiandaa siku kama siku yenu ya ndoa yaani ukaandaa sherehe f’lan, ukaalika marafiki ndugu na jamaa kisha ukampa zawadi mumeo.

Au unaweza ukaamua kumtoa ‘out’ kwa chakula kizuri kisha ukampatia kile ulichomuandalia.

Katika ‘speech’ yako ya siku hiyo mueleze mumeo au mkeo kuwa wewe huangalii mabaya mliyopitia bali unaangalia mazuri tu na umsifie kwa kuwa na wewe kwa siku zote.

Kabla ya sapraizi uliyomuandalia, siku hiyo mshukuruni Mungu kwa kusali pamoja kisha mueleze sababu ya kushiriki naye katika sala.

Hii najua haiwezi kutokea kila siku hasa kwa wanandoa wanaofanya kazi kila mtu ofisi yake kwa maisha ya hivi sasa lakini jitahidi kwa mwaka mara moja kuungana na mumeo kwenye sala kwa ajili ya kulinda ndoa yenu.

Leo naishia hapa, nimeona niwakumbushe wanandoa kufanya hili jambo ili kuboresha ndoa zenu.

Ishallah Mungu awafanyie wepesi kila kitu kiende vizuri.

Leave A Reply