The House of Favourite Newspapers

Sarpong: Nacheza Kwa Maelekezo Ya Kocha

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong, ameibuka na kusema hawezi kupoteza muda wake kuwafi kiria Sarpong: Nacheza kwa maelekezo ya kochawanaoponda kiwango chake na badala yake anaendelea kupiga kazi kuisaidia timu yake huku akifuata maelekezo ya kocha wake, Cedric Kaze anataka nini.

 

Sarpong ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa nayo manne aliyoyafunga katika mechi 12 alizocheza kabla ya kupambana na Mwadui.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Sarpong alisema jambo kubwa analoangalia kwa upande wake ni jinsi gani anapambana kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri na kufuata maelekezo ya Kaze.“

Nadhani suala la mashabiki kuzungumza katika soka ni jambo la kawaida, hilo haliwezi kunipa presha. Mimi naangalia jinsi gani naweza kuwa msaada katika timu kutokana na maelekezo ya kocha na kile ambacho timu inahitaji.“

 

Nafahamu suala la kufunga kwa mshambuliaji ni jambo la muhimu, kwa sasa nafanya kazi ile ambayo kocha anataka kuona ili tuendelee kutimiza malengo,” alisema Sarpong.

Stori na IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply