The House of Favourite Newspapers

Daktari Ashauri Watu Kutooga, Yeye Hajaoga Miaka 5

0

DAKTARI bingwa wa tiba ya uzuiaji wa magonjwa, James Hamblin, alifanya utafiti kuhusu utakatishaji wa ngozi ambao hivi karibuni umechapishwa katika kitabu.

 

“Ninajihisi vizuri kabisa,”alisema alipoulizwa anajihisi vipi baada ya kuishi bila kuoga kwa kipindi cha miaka mitano na kuongeza: ”Unazowea tu.”

 

Hamblin ana umri wa miaka 37, na ni mtaalamu aliyesomea taaluma yake katika Chuo Kikuu cha Yale kitengo cha Huduma ya Afya ya Umma na ni daktari bingwa wa tiba ya kuzuia magonjwa. Hata hivyo, anasisitizia juu ya umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni lakini anasema siyo lazima kuosha sehemu nyingine za mwili mara kwa mara.

 

Yeye ni mmoja wa waandishi wa jarida la Marekani -The Atlantic – ambamo aliandika taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosema: Niliacha kuoga, na maisha yangu yameendelea vyema.

 

“Tunatumia muda wa miaka miwili maishani mwetu kwa kuoga tu. Muda huo unaweza kuzalisha kiasi gani cha pesa na maji tunavyotumia katika kuoga, si vinapotea bure?” anasema katika taarifa yake katika katika jarida hilo la mwaka 2016.

 

Mwaka huu alichapisha taarifa nyingine yenye kichwa cha habari kinachosema: Unaoga kupita kiasi.

 

Hata hivyo anasisitiza kuwa watu wasiache kunawa mikono kwa sabuni,  pia anaamini kuwa hatupaswi kuoga sehemu nyingine za mwili mara kwa mara.

 

Alipoulizwa ni kwa nini aliacha kuoga, alijibu: “Kusema kweli ni hadithi ndefu,  inahitaji kuandika kitabu kuelezea ni kwa nini. Lakini nilitaka kujua ni nini kinachoendelea.

 

“Ninawafahamu watu wengi ambao wanaoga mara chache sana. Nilifahamu kuwa inawezekana, lakini nilitaka kujaribu ili nione kutooga kutakuwa na athari gani.”

 

Mwaka 2015, alifanya uamuzi. Ni nini alichokigundua? Na alipata athari gani?

 

”Baada ya kutooga muda mrefu mwili unazoea zaidi na zaidi kwa hiyo haunuki vibaya usipotumia sabuni au manukato.

 

“Na mwili wako haupati mafuta unapoacha kutumia sabuni kali. Lakini  jambo kubwa la kuelewa ni kwamba inachukua muda kuona athari hizi, hazijitokezi haraka, sio mara moja.

 

“Miili yetu ina uhusiano mkubwa na mfumo wa kinga ya mwili kwani huwa kiunganishi cha maisha ndani ya mwili na mazingira tunamoishi,” anafafanua.

 

Alisisitiza kuwa kwa upande wake mabadiliko ya kutonuka kwa mwili na kutoka jasho yalikuwa ya polepole: alianza kwa kutumia sabuni kidogo, shampuu na manukato na kuoga mara chache na akaendelea kufanya hivyo kila siku.

 

”Kulikuwa na wakati ambapo nilihisi ninataka kuoga kwa sababu nilihisi ninatamani kuoga na nilikuwa ninanuka vibaya. Lakini nikajitahidi kuendelea, na hisia ya kutaka kuoga ikatoweka ikawa ikinijia mara chahce sana,” anasema.

 

Miaka minne iliyopita

Taarifa aliyoiandika mwaka 2016 inasema: “Harufu ya mwili inatokana na bakteria wanaoishi kwenye ngozi zetu na kula mafuta yanayotolewa mwilini mwetu kwa jasho kwa njia ya vinyweleo.

 

“Tunashambuliwa mara kwa mara na vimelea, lakini si wote wanaotusababishia matatizo. Kujipaka mafuta katika mwili  na nywele kila siku huondoa aina ya uwiano baina ya mafuta na bakteria wanaoishi ndani yake.

 

“Unapooga kwa nguvu kila wakati, unaharibu bayoanuwai ambao huongezeka idadi yake haraka.  Lakini bayoanuwai hawa hawana uwiano na hupenda aina fulani ya vimelea ambao hutengeneza harufu ya mwili.

 

“Lakini, baada ya muda, mchakato wa udhibiti hufanyika.  Bayoanuwai yako hufikia kiwango cha kuwa thabiti na huwezi kunuka vibaya tena. Hutoi harufu kama ya ua  waridi.”

 

Kwa mujibu wa BBC katika mahojiano yaliyochapishwa mwaka huu katika wavuti wa Chuo Kikuu cha Yale, Hamblin alithibitisha kuwa siyo kwamba hakunuka lakini vimelea  mwilini mwake havikutoa harufu zaidi kuliko ya kawaida.

 

Leave A Reply