The House of Favourite Newspapers

‘SAUZI’ YAMWONDOLEA GRACE MUGABE HADHI YA KIDIPLOMASIA

Robert NA Grace Mugabe

MAHAKAMA moja nchini Afrika Kusini imeutupilia uamuzi wa serikali nchini humo wa kumpa mke wa  aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe, kumpa hadhi ya kidiplomasia katika kesi yake ya kumshambulia mtu, ambayo inaendelea jijini Johannesburg.

Jaji  Bashier Vally amesema kumpa hadhi hiyo mwanamke huyo ni kinyume cha katiba.  Kuna habari pia kwamba iwapo Mamlaka ya Mashtaka ya Taifa (NPA) ikishinikiza katika mashitaka hayo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 53 anaweza kupelekwa Afrika Kusini kukabiliana na kesi hiyo.

Mwaka 2017, mwanamitindo wa kike,  Gabriella Engels,  alimfungulia mashitaka Grace  kwa kumpiga na waya wa umeme baada ya kumkuta akiwa na mwanaye wa kiume.

Hata hivyo, Grace alikataa akisema Engels ndiye alianza kumshambulia na yeye alikuwa anajibu mashambulizi hayo kwa kujihami.

Wakati huo, idara ya mashitaka ya polisi nchini humo (SAPS) ilifanya uchunguzi lakini ikakataa kufungua mashitaka kwa vile  alipewa hadhi ya kidiplomasia na waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashaban, hivyo aliweza kurejea Zimbabwe.

Alichokisema COYO Msibani kwa Mama Shigongo

Comments are closed.