The House of Favourite Newspapers

Scrub ya vanilla, mafuta ya mzaituni kwa kutelezesha mwili

0

Wanawake wanapenda kuwa na muonekano mzuri, ndiyo maana wengi wao wanatumia gharama kubwa ili waonekane warembo.
Wiki hii nataka kukupa njia ambayo inaweza kuifanya ngozi ya mwili wako iteleze kwa kutumia scrub ya vanilla na mafuta ya mzaituni.

Mahitaji
Nusu kikombe cha sukari nyeupe iliyosagwa
Kijiko kimoja kikubwa cha asali
Nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni
Jinsi ya kufanya
Chukua sukari, changanya na mafuta ya mzaituni. Ukishachanganya vizuri, weka asali na vanilla.
Ukishapata mchanganyiko huo, upake mwilini mwako. Hii ni scrub nzuri, jitahidi kutumia kwa ajili ya kuifanya ngozi yako kuteleza na kuleta mvuto mpya.

Leave A Reply