The House of Favourite Newspapers

Selasini Asema Bado ni Mwanachama wa NCCR, Asema Hamtambui Simbeye

0
Joseph Selasini

 

Kufuatia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini, Mbunge wa zamani wa Rombo kwa tiketi ya Chadema ambaye baadaye alihamia NCCR Mageuzi, amesema yeye ni mwanachama halali wa chama hicho.

 

Kauli ya Selasini inakuja siku moja baada ya Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uhusiano wa NCCR, Edward Simbeye kueleza kwamba Selasini siyo mwanachama wa chama hicho kwa sababu hajalipia ada ya uanachama kwa takribani miaka miwili.

 

Joseph Selasini, Mbunge wa Zamani wa Rombo

 

Selasini ameyasema hayo wakati akihojiwa kwa njia ya simu kupitia Kipindi cha front Page kinachorushwa na +255 Global Radio na Global TV na kueleza kuwa kikao cha halmashauri kuu kilivunja safu yote ya uongozi wa chama hicho hivyo hamtambui Simbeye kama Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mawasiliano ya NCCR.

 

Siku chache zilizopita, NCCR Mageuzi kiliingia kwenye mvurugano mkubwa baada ya baadhi ya wanachama wa chama hicho, kutangaza kumsimamisha Mwenyekiti, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara.

Leave A Reply