The House of Favourite Newspapers

Selcom na NALA Wanaungana Kurahisha na Kuleta Unafuu Miamala ya Pesa Tanzania

0
Benjamin Fernandes, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NALA akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi ya kutuma pesa kutoka Tanzania kwenda nje ya Marekani na Uingereza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya Selcom na NALA jijini Dar es Salaam tarehe 28 Juni 2022. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Sameer Hirji wa Selcom.

 

 

DAR ES SALAAM, 28 Juni 2022: Selcom na NALA zimeingia makubaliano ya kushirikiana ya kuongeza nguvu ya kutuma fedha nchi za nje kwenda Uingereza na Marekani moja kwa moja kupitia miamala ya simu za mkononi na akaunti za benki.

 

Selcom ambao ni watoaji huduma wakubwa wa malipo nchini Tanzania, wametangaza ushirikiano huo wa kimkakati na NALA, kampuni ya kivumbuzi yenye makao yake makuu nchini Uingereza, utakaowezesha kuchochea miamala ya moja kwa moja kutoka nchi hizo mbili wakati wowote.

Sameer Hirji, Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom (Kushoto), akiwa na Benjamin Fernandes, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NALA (Kulia), wakitia sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya kampuni hizo mbili katika kutoa huduma za kutuma fedha nchi za nje kwenda Tanzania, tukio lililotokea DSM tarehe 28 june.

 

 

Ushirikiano na Selcom unasaidia kuiweka NALA katika mstari wa mbele katika kasi ya mapinduzi ya utumaji pesa ndani na nje ya nchi. Kasi hii ya mapinduzi inapewa nguvu kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Selcom katika ikolojia ya huduma za kifedha kama njia muhimu na uwezo wa NALA katika uvumbuzi bora wa bidhaa na huduma.

 

Kwa ushirikiano huu, watumiaji wa NALA nchini Uingereza na Marekani sasa wanaweza kuhamisha fedha kwenda benki kadhaa na kufanya miamala ya simu za mkononi nchini Tanzania kwa urahisi popote walipo. Hii pia itawapa Watanzania waishio ughaibuni fursa ya kutuma mitaji nchini. Mwaka 2021, Tanzania ilipokea dola milioni 570 kama fedha kutoka nje ya nchi, kutoka dola milioni 400 mwaka 2020.

Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Selcom na NALA kwenye uzinduzi wa ushirkiano kati ya kampuni hizo mbili kwenye kutuma fedha nchi za nje.

 

 

Mwaka 2022, Selcom inatarajia kufanyakazi kwa karibu na NALA, Serikali na mashirika mingine ili kukuza mapato zaidi kupitia uwekezaji katika sekta kama vile elimu, afya na kilimo. Wakati huo huo, NALA inaendelea kuendeleza dhamira yake ya kukuza fursa za kiuchumi kwa Afrika kwa kujenga masuluhisho nyeti ya kifedha.

 

Katika maelezo yake, Sameer Hirji, Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom,     alisema,  “tunafuraha kushirikiana na NALA, chapa iliyoanzishwa katika dhamira ya kuongeza fursa katika bara la Afrika na kwa Wanadiaspora duniani kote. Kupitia uzoefu na uwezo wetu kama Selcom itakuwa nyongeza muhimu na ya kimkakati kudumisha huduma za kifedha nchini kushirikiana na huduma za kifedha za kijamii kutoka NALA.

 

Aliendelea kusema, ‘ushirikiano wetu utawawezesha wateja wa NALA kutuma pesa kwa njia ya uwazi na ufanisi, hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wateja wa NALA nchini Tanzania na kuunda njia mpya ya utumaji fedha kwa watu wanaoishi nje ya Afrika ili waweze kutuma pesa nyumbani na kwa msaada wa Benki Kuu na washirika kama vile NALA tunatarajia kuleta matokeo yanayoonekana.”

 

Benjamin Fernandes, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendajiwa NALA aliongeza kuwa, “Ushirikiano na Selcom ni ishara ya nia yetu ya kuimarisha uwepo wa NALA katika masoko tuliyoyapa kipaumbele.

 

Kama Mtanzania, inanifurahisha sana kuwekeza katika nchi yetu na ughaibuni. Aliendelea, ‘Afrika  ndilo bara ghali zaidi duniani kutuma pesa, na lengola NALA ni kubadilisha dhana hiyo kwa kuunda masuluhisho ya kifedha ambayo Waafrika wanastahili. Na tunapozidi kupanua bidhaa zetu ili kuwafikia watu wengi zaidi, inakuwa muhimu zaidi kupata washirika muhimu ili kutimiza azma hii’.

 

Kupitia ushirikiano huu mpya inaendelea kuiweka Selcom kama chaguo sahihi kwa kampuni bunifu kama vile NALA kuzidi kukua kwasababu ya uwezo wa Selcom kujenga miundombinu ya malipo ya kifedha kimataifa ambayo pia inaunganisha taasisi za fedha kama vile benki na simu za mkononi kirahisi na kwa uaminifu.

 

Makampuni yote mawili yanaamini kuwa ushirikiano huu wa mwanzo ni kiashiria tosha kudumisha safari mapinduzi katika tasnia ya utumaji fedha nchini Tanzania na sambamba na kukuza upokeaji wa fedha kutoka nchi za nje.

About Selcom:

Selcom is a Pan African financial and payment services provider, offering a comprehensiverange payment, issuing andacquiring services.

About Nala:

NALA is an African payments company which also has a money transfer app that enables you to make secure and reliable payments from the UK and the United Statest of Africa in seconds.

 

They are on a mission to increase economic opportunity on the African continent and its diaspora worldwide. Creating community-powered financial solutions make site asier to make day-to-day payment sand dobusinessinan increasingly global Africa.

Payments in Africa are 1% built. NALA aspires to bring 21st-century payment technology toAfrica to create a low-cost and highly reliable set of payment rails that friends, family, and business escanuse. When payment sare simple, reliable, and available at the touch of a button, any thing is possible.

Leave A Reply