The House of Favourite Newspapers

Sensa ya Watu na Makazi 2022, Jiandae Kuhesabiwa Kesho

0
Sensa ya watu na makazi inafanyika kesho Agosti 23, 2022

IKIWA imesalia siku moja kabla ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza zoezi la kitaifa la Sensa ya Watu na Makazi kesho tarehe 23 Agosti 2022, viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini na wananchi kwa pamoja wanaimba wimbo mmoja, kuhamasisha kila mmoja kujiandaa kuhesabiwa.

 

Madhumuni ya sensa ya sita ya watu na makazi tangu uhuru ni kutoa taswira wazi kuhusu idadi ya watu na hali ya maisha ya nchi. Kila baada ya miaka kumi, Tanzania hufanya hesabu ya idadi ya watu, na sensa ya kesho itakuwa ya sita katika mfululizo ulioanza mwaka wa 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka wa 1967, 1978, 1988, 2002, na 2012.

Sensa ya Makazi pia itafanyika kesho Agosti 23, 2022

Sensa ya watu inafanywa ili kuwezesha serikali kuwa na taarifa za watu wake, idadi ya watu, muundo wa umri na jinsia, na sifa nyingine muhimu za kijamii na kiuchumi. Na la zaidi kwa mara ya kwanza, taarifa zitakusanywa kwa njia ya kidijitali kwenye vifaa kama vile kompyuta za mkononi badala ya kwenye karatasi, ambayo mamlaka inasema itahakikisha faragha zaidi na usindikaji wa haraka.

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply