The House of Favourite Newspapers

Babu Tale: Rayvanny Hajakamilisha Utaratibu, Bado ni Mali ya WCB

0
Babu Tale akiwa pamoja na Diamond Platnumz

MMOJA wa mameneja wa Lebo ya WCB, Hamisi Taletale, ‘Butale’ ameweka wazi kuwa msanii Rayvanny bado yupo chini ya #WCBWASAFI kwa sababu bado hajakamilisha utaratibu wa kujiondoa katika lebo hiyo.

 

Babu Tale ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha #BigSundayLive cha Wasafi TV ikiwa ni miezi kadhaa baada msanii huyo kutangaza kuwa amejiondoa rasmi WCB.

 

“Rayvanny amekua amekuja Wasafi akiwa hana uwezo akafanya biashara na Wasafi na sasa hivi ana majumba na anajiweza na amefungua record label yake, leo hii #Rayvanny anataka kwenda kuendelea na biashara yake mwenyewe.

 

“Biashara iko wazi na ruhusa ya kununua haki/hisa zake kwetu ndio hicho tunachokisubiria kikamilike, yupo kwenye mchakato ila tumempa uhuru wa kufanya kazi zake mwenyewe.

Babu Tale amesema Rayvanny bado ni mali ya WCB kwani hajakamilisha taratibu

“Kama hivi mnaona tumemruhusu anafanya show mwenyewe kila kitu mwenyewe kwa hiyo tunasubiria kila kitu kikamilike anakwenda kujitegemea kwahiyo ni vitu ambavyo vipo kwenye utaratibu.

 

“Vanny wakati anaenda Wasafi hajaenda kusaidiwa ameenda kufanya biashara na biashara yake imekuwa anakwenda kuwasaidia kina #Macvoice (bado hajamalizana na Wasafi) ni utaratibu tu ujue kumalizana sio kama taa paap kwasababu bado kila kitu kipo chini ya wasafi mpaka leo,” amesema Babutale.

Leave A Reply