The House of Favourite Newspapers

Serengeti Boys ni kufa na kupona Taifa

KOCHA Mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kuwa michezo yao miwili iliyobaki dhidi ya Uganda na Angola ni ya kufa na kupona. Katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon U17) inayoendelea jijini Dar, Serengeti Boys ipo Kundi A na timu za Nigeria, Angola na Uganda na tayari imeshapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria.

 

Katika kundi hilo, mpaka sasa Nigeria na Angola ndizo zimepata ushindi katika michezo yao ya kwanza huku Serengeti Boys na Uganda zikipoteza michezo yao ya kwanza.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mirambo alisema; “Lengo letu ni kufuzu Kombe la Dunia na ili ufuzu unatakiwa ushinde michezo miwili na ukiangalia ndio hiyo miwili tuliyobakiza dhidi ya Uganda na Angola, hivyo ni lazima tupigane kufa na kupona kuhakikisha tunashinda michezo yote miwili iliyobaki.”

 

Katika kundi hilo, Serengeti Boys inashika nafasi ya tatu , huku Nigeria ikiongoza ambapo leo Jumatano Serengeti itacheza dhidi ya Uganda na Angola dhidi ya Nigeria. Mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Comments are closed.