The House of Favourite Newspapers

Serengeti Music Festival Yafana Dodoma

0

USIKU wa kuamkia leo Februari 7, 2021, limefanyika bonge moja la tamasha pale makao makuu ya nchi, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, likikutanisha wasanii zaidi ya 70 kwenye jukwaa moja.

 

Tamasha hilo linaloandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, linafahamika kama Serengeti Music Festival au Tamasha la Vipaji, lilianza majira ya saa 1:00 usiku

Wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA, ambaye aliwakosha mashabiki wake na ngoma ya Gwiji.

Wasanii kama Madee, Tunda Man, Nandy, Shilole, Snura, Whozu, Z-Anto na wengine wengi walipita jukwaani kutoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na kanda ya kati kwa ujumla.

Pia Waziri wa Habari Innocent Bashungwa alikuwepo pamoja na Naibu Wake Abdallah Ulega, mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde, mbunge wa Shinyanga mjini Patrobas Katambi na wengine.

Leave A Reply