The House of Favourite Newspapers

Serengeti: Wanawake Walalamikia Kuolewa na Kaburi

0

Baadhi ya wanawake wa Wilaya ya Serengeti wamelalamikia utamaduni wa kuolewa na makaburi ambao bado upo hadi sasa kwa baadhi ya makabila mkoani Mara.

 

 

Ndoa za Makaburi ni kuwa kijana aliyefikia umri wa kuoa akifariki bila kuoa familia humuolea na watoto watakaozaliwa huitwa kwa jina la aliyefariki. Suala hilo hufanyika kwa siri ambapo anayeolewa haambiwi.

 

 

Msichana huolewa kwa muda na aliyemuoa humuacha na kuoa mke mwingine. Mwanamke aliyeachika anaweza kuzaa na mwanaume mwingine lakini watoto wataitwa jina la aliyefariki ambaye huhesabika kuwa ndiye aliyemuoa.

 

 

Katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Wanawake katika Wilaya ya Serengeti wamesema hatua za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuwanusuru.

Leave A Reply