The House of Favourite Newspapers

Serengeti Yatambulisha Tamasha La Oktoba 2023 Linalolenga Kusherekea Tamaduni Za Kitanzania

0
Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu SBL, Anitha Msangi Rwehumbiza akizungumza kwenye uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika Coco Beach jijini Dar.

Dar es Salaam, Tanzania–September 20, 2023. Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) inafuraha kutangaza tamasha la Oktoba Fest, linalolenga kusherekea tamaduni za kitanzania lililopangwa kufanyika tarehe 21 Oktoba 2023. OktobaFest 2023 inatarajwa kuwa tukio la pekee ambalo linaunganisha watu mbalimbali ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za Tanzania.

OktobaFest Tanzania ni sherehe ya kipekee inayojumlisha vyakula, muziki na utamaduni za Kitanzania. Watu wanaweza kutarajia nakshi za kipekee kupitia ladha ya vyakula tofauti na vibanda vingi vya vyakula vitavyohudumia vyakula vitamu vinavyoakisi ladha mbalimbali za kitanzania. Kuanzia vyakula vitamu vya kitamaduni hadi ubunifu wa kisasa wa mchanganyiko, Oktoba Fest ni tukio pekee la kitamaduni.

Meneja wa Chapa wa Serengeti Breweries, Esther Raphael akiwaeleza wanahabari (hawapo pichani) jinsi tamasha hilo linavyotarajiwa kufanyika. Kushoto ni Rispa Hatibu,
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL.

Safu ya muziki wa tamasha hili ni mchanganyiko wa midundo ya kitamaduni na midundo ya kisasa, inayoshirikisha wasanii wa aina mbalimbali nchini Tanzania. Wasanii hawa watapanda jukwaani ili kuonyesha sauti zao za kipekee, kuonyesha uzoefu wa muziki usiosahaulika kwa wahudhuriaji.

Pamoja na hayo, muziki, maonyesho ya dansi, sanaa na mitindo yataangazia urithi wa kitamaduni wa Tanzania, na kutoa uzoefu wa kusherekea utofauti wa kanda. Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti alisema kuwa, “OktobaFest sio tu sherehe ya utamaduni, lakini inalenga kuleta matokeo chanya katika sehemu zote muhimu ya jamii yetu. Serengeti Breweries imejitoa kwa dhati kuleta matokeo chanya kwa jamii inayohudumia.

Shamrashamra za uzinduzi wa tamasha hilo.

Tamasha hili litawasaidia wajasiriamali na wasanii kupata ustawi katika Nyanja zao zinazokuza za ujasiriamali, ubunifu na uendelevu”.

Kama wadhamini wa tamasha hilo, Serengeti Breweries inania kuhamasisha utamaduni wa mtanzania. Kutoka chakula, mitindo na sanaa, OktobaFest inalenga wasanii wachanga kwa kutoa jukwaa kwa vipaji vinavyoibuka ili kuonyesha ubunifu wao na ustadi wa mapishi, kukuza ujasiriamali na ubunifu.

Pamoja na haya, tamasha hili litajumuisha michezo mbalimbali inayounganisha teknolojia na mila, kutoa mtazamo wa pekee juu ya utamaduni wa kitanzania. Zaidi ya hayo, OktobaFestya SBL inachukua hatua muhimu ili kupunguza athari kwenye mazingira.

Wanamitindo waliovalia kiasili nao walinogesha uzinduzi wa tamasha hilo.

Juhudi kama vile udhibiti na utupaji ovyo wa taka na mbinu endelevu zitawekwa ili kuhakikisha usafi wa mazingira katika tamasha hili.                                                                                                                                        #SerengetiOktobafest
#ThisIsHowWeDo

Kuhusu SBL:

Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuniya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya Zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.

SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji iliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka.

Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za ajira kwa watu wa Tanzania. 

Chapa za SBL zimepokea tuzo nyingi za kimataifa zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness Stout, na Guinness Smooth. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnniew Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don – SBL’S maiden local spirit brand na Smirnoff Orange. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na: 

Rispa Hatibu,

Meneja Mawasiliano na Uendelevuwa SBL,

Simu: +255 685260901

Barua Pepe: [email protected]                                                                                                      

Leave A Reply