The House of Favourite Newspapers

Serikali: Idadi Wagonjwa #Covid-19 Tanzania Yapungua – Video

0


KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe amesema idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa huo kwenye baadhi ya vituo vya matibabu imepungua na wengi wao wanaendelea vizuri.

 

 

Amesema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa kinga vyenye thamani ya Yuan 2,150,00 sawa na shilingi 700,759,268 kutoka serikali ya China.

 

Ametaja idadi ya wagonjwa kwa siku kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani katika Hospitali ya Amana kuna wagonjwa 12 Kisoka, Mloganzila 6  na Kituo cha Kibaha chenye wagonjwa 24.

 

Msaada huo umetolewa leo katika Bohari ya Dawa (Medical Stores Department) ambapo alisema msaada huo umekuja wakati mzuri kwani utawasaidia watumishi wa afya katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona  yanayosababisha homa ya Covid-19.

“Niwaombe na niwasisitize wafanyakazi wa afya, mjitahidi kuwahudumia watu wenye magonjwa mengine huku mkiendelea kutekeleza wajibu wetu kwa wagonjwa wa Covid-19.

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Gabriel Mhidze, ameishukuru kwa kupatiwa msaada huo kutoka China na ameahidi kwamba utasambazwa kwa walengwa kama ilivyokusudiwa.

 

“Nashukuru Serikali ya China kwa msaada huu, hivi sasa naweza kusema bohari yangu ina vifaa vya kutosha kusambaza kwa walengwa wote nchini,” amesema.

 

Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Wang Ke amesema Serikali yake ya China imetoa barakoa 12,000, ‘gloves’ 10,000, viatu 10,000 pamoja na vifaa kinga mbalimbali kwa ajili ya wataalamu wa afya.

 

“Ni matumaini yangu kwamba msaada huu ambao tumeutoa leo, utasambazwa kwa watalamu wa afya ili wavitumie wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wa Corona na hivyo kuokoa maisha yao,” amesema.

Naye Balozi Wang Ke amemshukuru Rais John Pombe Magufuli pamoja na Serikali yake kwa msaada mkubwa iliyotoa kwa raia wa China baada ya kuibuka kwa janga la ugonjwa Covid-19 na hivyo kuleta nguvu ya pamoja katika kukabiliana na ugonjwa huu.

 

“Kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na janga hili la ugonjwa wa  Corona, ili kulinda maisha ya watu wake, napenda kusema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika mapambano haya,” amesema.

 

Amesema China na Afrika zinapaswa kuendelea kushirikiana katika kupambana na ugonjwa wa huo, huku jumuiya ya kimataifa ikiendelea kutoa ushirikiano katika janga hili.

Leave A Reply